Choose the page language

Katika kipindi hiki, Your Story’s Wakili mkuu, Sifa Mtango anaelezea jinsi watu wenye ulemavu wanavyoweza kupata usaidizi wa kisheria wa bure na huru ili kushiriki hadithi yao na Disability Royal Commission, na kuunganishwa na huduma za ushauri na utetezi. The Disability Royal Commission inaendelea hadi Septemba 2023.

Your Story Disability Legal Support ni huduma bure ya msaada wa kisheria ya huru ambayo inapatikana kwa watu wenye ulemavu wanaotaka kushiriki hadithi yao na Disability Royal Commission. Familia za watu wenye ulemavu, watunzaji, wasaidizi na wakilishi wa watu wenye ulemavu wananotaka kushiriki hadithi yao wanaweza pia kupata ushauri ya kisheria kutoka Your Story.

Ili kupata maelezo zaidi au kutumia Your Story, piga simu kwenye 1800 77 1800 Jumatatu hadi Ijumaa (simu bure) au nenda kwenye kurasa ya tuwasaliana nasi kwa njia nyingine za kufikia kwenye Your Story Disability Legal Support.

Kwa maelezo zaidi tafadhali tembelea https://yourstorydisabilitylegal.org.au
 

About the guest speaker

Mzungumzaji Mgeni wetu ni Sifa Mtango, Wakili Mkuu wa Your Story Legal Support (Legal Aid NSW). Bi Mtango ni wakili mtaalamu wa kutatua mizozo na anaye uzoefu wa zaidi ya miaka 10.

Interview by
Joy Rahab Sinclair

Joy Rahab ni mwanamke mzaliwa wa Kenya mwenye umri wa miaka 42 mwenye watoto watatu. Alikuja Australia kama mwanafunzi mwaka 2005. Ana digrii mbili katika Sheria zilizopatikana nchini India, vyeti... Go to page where you can read more about Joy Rahab Sinclair